เนื้อเพลง Isaya 49: 14-16
Isaya 49: 14-16 - Pastor Abiudi Misholi
Nasoma katika kitabu cha Isaya 49 na
Ule mstari wa 14 hadi wa 16 Biblia inasema hivi
Sayuni alisema Yehova ameniacha
Bwana amenisahau
Je mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyae
Hata asimuhurumie mwana wa tumbo lake
Naam hawa waweza kusahau
Lakini mimi sitakusahau wewe
Tazama nalikuchora katika vitanga
Vya mikono yangu na kuta zako ziko mbele zangu daima
Ndugu msikilizaji nataka nikwambie siku
Ya leo iko sauti ambayo imeongea masikioni mwako
Ya kwamba Mungu amekuacha na tena
Amekusahau na wala hajakuona
Hata mimi nimeshawahi kupita katika kipindi hichi
Nikaona kwamba Mungu ameniacha tena
Mungu amenisahau
Hata nikatamani nijitupie kwenye gari nigongwe nife
Lakini ikaja sauti nyingine kusema ya kwamba
Mungu hajanisahau tena Mungu hajanicha na
Mungu yuko pamoja nami
Ngoja nikwambie neno la leo
Sayuni wakalalamika
Wakasema Bwana umetuacha na Yehova ametusahau
Mungu akawauliza swali moja
Je mwanamke anaweza
Akamsahau mtoto wake anyonyaye asimuhurumie mwana
Wa tumbo lake
Lakini Mungu akajibu ilo swali tena yeye mwenyewe
Akasema mwanamke anaweza akamsahau mtoto wake
Lakini mimi sitakusahau wewe
Maana nimekuchora katika vitanga vya mikono
Yangu na kuta zako ziko mbele yangu daima
Wanawake wengi leo hii
Wanazaa watoto wao wanawatupa kwenye majalala
Wengine wanazaa watoto wao wanawauwa kwa siri
Wengine wanawatupa katika mashimo ya choo
Lakini Mungu anasema hawezi kukusahau wewe
Wengine wakawazaa watoto wao wakawapeleka kwa bibi zao
Hata misaada hawapeleki
Maana wamewasahau
Lakini Mungu anasema hawezi kukusahau wewe
Hawezi kusahau kazi yako
Hawezi kusahau watoto wako
Hawezi kusahau uaminifu wako
Ondoa ilo wazo la sikio la pili
Ambalo linasema Mungu amekusahau
Ilo linatoka kwa shetani wala halitoki kwa Mungu
Lakini Mungu anasema leo hawezi kukusahau wewe
Hawezi kukusahau mama yangu
Hawezi kukusahau baba Yangu
Hawezi kukusahau kijana
Hawezi kukusahau dada
Amekuchora katika mikono yake na kuta zako ziko mbele yake daima
Ebu weka mkono wako sasa mahali panapouma ukiwa
Una shida yeyote inakusumbua weka mkono moyoni mwako
Iwe unamatatizo mbali mbali naenda kukuombea sasa
Katika jina la Yesu Kristo mwana wa
Mungu uliyeketi mahali pajuu palipoinuka
Naenda kinyume sasa na kazi za shetani
Nakwenda kinyume na nguvu za giza
Nakwenda kinyume sasa na mamteso yote yanayokusumbua
Nayaamuru yatokeee kwa Jina la
Yesu Mungu aliye hai
Nayaamuru yatoke yarudi huko yalikotoka
Ukawe mzima baba
Ukafanikiwe kwenye kazi zako
Ukafanikiwe kwenye ndoa yako
Ukafanikiwe kwenye shughuli zako
Ukafanikiwe kwenye vitu vyako na masomo yako
Mungu akukumbuke na akubariki nakutakia maisha mema
Katika jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai
Ukawe mzima
Hutanisahau
Hutanisahau
Hutanisahau baba
Wewe Mungu wewe wa huruma
Hutanisahau hutanisahau
Hutanisahau hutanisahau
Yesu hutanisahau hutanisahau
Hutanisahau wewe Baba wewe
Wewe Mungu wa huruma
Hutanisahau Ninakuabudu Yesu ninakuabudu
Ninakuabudu ninakuabudu Yesu Nakuabudu Baba
Ninakuabudu ninaaakuabudu wewe Baba
Wewe Mungu wa Huruma wa huruma ninakuabudu
Ninakuabudu
Ninakuabudu tena Messiah Messiah
Ninakuabudu
Ah ah Nakuabuuuduu Yesu wee
Ninakuabudu Halelu halelu halelu
Haleluuu nakuabudu Baba
Ewe Mungu ewe Mungu wa huruma
Wa huruma ninakuabudu
Nakutakia maisha mema maisha ya amani na maisha ya furaha
Ubarikiwe na watoto wako ulindwe kazini mwako
Uinuliwe sana ufutwe machozi
Pokea haja ya Moyo wako kwa jina La Yesu Nakubariki
Amen
Amen
เกี่ยวกับเพลงนี้ :
เพลงนี้ถูกปล่อยออกมาในวันที่ 30 เม.ย. 2013, เพลง Isaya 49: 14-16 จาก Pastor Abiudi Misholi ที่ร่วมกันสร้างสรรค์ท่วงทำนองและเนื้อร้องได้ยอดเยี่ยม
ดาวน์โหลด JOOX Application และ รับฟังเพลง, ชมมิวสิควีดีโอ และอ่านเนื้อเพลง แบบออนไลน์ได้ทุกที่ทุกเวลา
Tags ที่เกี่ยวข้อง :
Isaya 49: 14-16 (โดย Pastor Abiudi Misholi), Isaya 49: 14-16, Isaya 49: 14-16 มิวสิควีดีโอ, Isaya 49: 14-16 เนื้อเพลง, Pastor Abiudi Misholi เพลง